Kwa kuona umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii, nimeona vema kuungana na kampeni maalumu ya uhamasishaji ya UNFPA na Prezi yenye jina #YouthAgainstCOVID19. Nimetumia lugha adhimu ya Kiswahili ili kuwasaidia wale ambao kampeni hii inaweza isiwafikie kwa lugha wanayoielewa. Ni matumaini yangu kuwa elimu hii fupi na ushauri niliotoa utatusaidia sote. Pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kazi nzuri inayofanya, na pongezi kwako kwa kuendelea kujilinda na kuwalinda uwapendao. Kongole sana!